Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Vikosi vya serikali ya Syria vikisaidiwa kwa mashambulizi ya ndege za kivita za Urusi na kuongozwa na wataalamu wa vita kutoka Iran, vimeendelea kupambana na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh kuelekea mji wa wenye utajiri wa mafuta wa Deirezzor.
Vikosi hivyo vinazidi kusonga mbele kuelekea kwenye jimbo la Deir Ezzor, ambalo ni ngome ya kundi la kigaidi la Daesh, siku moja baada ya kuchukua tena udhibiti wa mji wa kale, Palmyra, ambao majengo yake yalibomolewa na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh. Rais wa Syria, Bashar al-Assad amesema kukombolewa mji wa Palmyra kutoka kwa wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh ni ushindi mkubwa katika mapambano ya kimataifa dhidi ya ugaidi duniani.
Iran, mshirika mwingine muhimu wa Rais Assad, imepongeza hatua ya kukombolewa mji wa Palmyra na imeahidi kuendelea kuisaidia Syria kifedha na kijeshi. Jeshi la Syria limesema mji huo uliokombolewa utatumika kama makao mapya ya kuendesha operesheni dhidi ya ngome imara za kundi la kigaidi la Daesh mjini Raqqa na Deir al-Zor.
Shirika linalofatilia haki za binaadamu nchini Syria lenye makao yake Uingereza, limesema mapambano yameendelea kaskazini mashariki mwa Palmyra kuelekea Deirazol kati ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh wanaodhaminiwa na Saudia arabia na vikosi washirika kwa serikali, vikisaidiwa na jeshi la wanaanga la Syria na Urusi na wanajeshi wa ardhini wa Iran. Kwa mujibu wa shirika hilo, mashambulizi ya anga pia yaliilenga barabara inayotumiwa na magaidi kutoka Palmyra inayoelekea mashariki mwa Deir al-Zor na mapigano yanaendelea kwenye mji wa Qaryatain unaoshikiliwa na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh. Serikali ya Syria imekuwa ikijaribu kuukomboa mji wa Qaryatain tangu ulipotekwa na IS mwezi Agosti mwaka uliopita.
Marekani yahofia utawala wa Assad
Marekani ambayo kwa muda mrefu imekuwa iwasaidia waasi na magaidi nchini Syria imepongeza hatua iliyofikiwa na vikosi vya Syria kwa tahadhari, huku msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, John Kirby akisema nchi yake haifikirii kwamba ushindi huo dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh utakuwa ufumbuzi wa muda mrefu. Marekani pia imedai kuwa inahofia rekodi ya utawala wa kikatili wa Rais Assad.
''Tunadhani ni jambo zuri kwamba magaidi wa kundi la kigaidi la Daesh hawana udhibiti tena. Lakini bila shaka tunatilia maanani kwamba njia bora kwa Syria na watu wa Syria siyo kuongeza uwezo wa Bashar al-Assad kuendeleza utawala wa kikatili kwa watu wa Syria,'' alisema Kirby.
Kukombolewa kwa mji wa Palmyra ni pigo kubwa kwa kundi hilo la kigaidi, tangu lilipojitangazia uongozi wa ukhalifa mwaka 2011 katika maeneo mengi ya Syria na Iraq na ni mapinduzi makubwa kwa Syria na Urusi.
Pia ni pigo kubwa kwa Marekani na washirika wake ambao wamekuwa wakiyasaidia makundi ya kigaidi ili kuiangusha serikali halali ya Syria.
Kundi la kundi la kigaidi la Daesh limeuharibu mji huo kwa kuyabomoa makaburi na mahekalu kadhaa, wakati wa udhibiti wake wa miezi 10 ambao walisaidia na Marekani na washirika wake. Mji huo uko katika orodha ya turathi za dunia za shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni-UNESCO na unajulikana kama 'Lulu ya Jangwani'.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry amedai kuwa nchi yake itaongeza kile alichokisema kuwa ni shinikizo zaidi dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh baada ya kukutana na waziri mwenzake wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu mjini Washington.
Marekani na Uturuki zimekuwa zikilisaidia kundi la kigaidi la Daesh ambapo Uturuki imekuwa ikilitumia kundi hilo kuwaua wakurdi na Marekani imekuwa ikilitumia kundi hilo kuiangusha serikali halali ya Syria, huku nchi hizo mbili zikijinadi kuwa zinapambana na kundi la kigaidi la Daesh.
Mwisho wa habari/ 291